Njia rahisi ya kutenengeneza biskuti

Image result for namna ya kutengeneza biskuti
Biskuti

Ipo njia rahisi sana ya kutengeneza biskuti nzuri na tamu sana kwa kutumia mahitaji matatu tu. Ni pishi rahisi sana na waweza kutumia jiko la oven au jiko la mkaa wa kawaida.
MAHITAJI

  • Mafuta ya Butter au Blue Band kiasi ya robo kg
  • Sukari ile laini robo
  • Na Unga wa baking (All purpose flour)
CHAKUFANYA.
  • Kwanza changanya butter/blueband na sukari – vichanganye hadi vilainike kabisa, 
  • kisha ongeza unga wa baking hapo pia changanya sana vya kutosha hadi unga uwe umeshikana kumbuka mahitaji ni hayo matatu usiongeze maji. 
  • Baada ya kuwa umeuchanganya vema unga wako uhifadhi kwa friji au mahali tulivu kwa dakika 20 hivi. 
  • Pasha jiko lako moto kama watumia oven au kama ni mkaa uwe tayari.
    Baada ya hapo toa na ukande upya kisha tengeneza katika shape za biskuti unazozipenda. 
  • Weka katika baking sheet kwa wanaotumia oven – weka katika oven biskuti zako – 
  • usiwe mbali na jiko kwani ndani ya dakika 15 – 20 zinatakuwa tayari pale utakapoona zinaanza kuwa brown katika kona na biskuti. 
  • Zikiwa tayari wazitoa na kuacha zipoe kwa dakika 5 basi hapo zipo tayari.

Comments

Popular Posts