Je unajua kuwa Facebook itaanza kufundishwa kama somo India!
Wanafunzi India wakitumia facebook |
Kuandika ujumbe na kupakia picha na
video limekuwa jambo la kawaida kwa karibu watu bilioni mbili wanaotumia
mtandao wa kijamii wa Facebook.
Ingawa ujumbe wako wa siasa au
salama za heri, pongezi au rambirambi unaweza kupendwa na wenzako, si
wengi wanaoweka kuchukulia ujumbe huo kuwa fasihi au kazi ya sanaa.
Lakini sasa Chuo Kikuu cha Delhi (DU) kimechukua msimamo tofauti.
Kinataka kujumuisha kuandika ujumbe wa Facebook kuwa sehemu ya mtalaa wake wa somo la Kiingereza.
Wanafunzi watakuwa wakifunzwa pia jinsi ya kuandika blogu au barua kuu ya kujitambulisha wakati wa kuwasilisha maombi ya kazi.
Delhi University (DU) ni miongoni mwa vyuo vikuu bora zaidi nchini India. Watu maarufu wengi wameshawahi kusoma katika chuo hicho.
Miongoni mwa waliowahi kusomea katika chuo kikuu hicho ni waziri mkuu
Narendra Modi na kiongozi wa Burma na mshindi wa Tuzo ya Amani ya
Nobel Aung San Suu Kyi.
Mambo hayo yamejumuishwa kwenye mswada wa mtalaa wa Kiingereza ambao unatathminiwa na maprofesa wa DU.
Prof
Christel Devadawson, mkuu wa kitivo cha lugha ya Kiingereza aktika chuo
kikuu hicho, alisema kwamba ujumbe kwenye Facebook utatumiwa kama
sehemu ya Kozi ya Kuimarisha Ujuzi - ambayo ni sehemu ya somo
inayotumiwa kuwapa wanafunzi maarifa na ujuzi wa kuwawezesha kufaa
maeneo ya kazi.
Gazeti la Hindustan Times linasema nchini India,
mitandao ya kijamii inaweza kumzolea umaarufu mkubwa mwandishi chipukizi
au msanii na kumuwezesha kufikia watu wengi au hata kupata mkataba wa
kuchapisha kazi zake.
Comments
Post a Comment