Jifunze jinsi ya kuandaa burger ya nyama ya ng'ombe
Utakachohitaji ni:
- Nyama ya kusaga
- Tango
- Unga wa mkate
- Kitunguu swaum kilichosagwa
- Kitunguu maji
- Tangawizi iliyosagwa
- Nyanya
- Yai moja
- Lettice
- Chumvi
- Mayonnaise
- mikate ya burger 3
- ketchup.
Tia minofu ya nyama ya ngo'ombe kwenye bakuli kisha weka chumvi, unga wa mkate, yai,
kitunguu swaum,tangawizi na kitunguu maji na kisha uichanganye vizuri na uitawanyishe katika madonge 3
Baada ya hapo iache ikae kwa muda wa dakika 30 na itakuwa tayari
kwa kupikwa. Pika upande mmoja mpaka uive na
kisha ugeuze upande wa pili na pia uupike mpaka uive katika moto mdogo.
Beef Burger |
Ikiwa
hauna jiko la mkaa unaweza kutia kwenye oven na uiache kwa muda wa
dakika 15 au 14ukiigeuza kila upande kwa kitambo mpaka itakapoiva.
Baada
ya hapo andaa mkate wa burger kwa kuukata kati kisha katakata tango, kitunguu,nyanya na lettice.Kisha anza kuvipanga kwenye mkate wa
burger kwa kuweka lettice chini kisha tango,nyanya, vitunguu na kisha
burger yenyewe. Baada ya hapo tia mayonnaise na ketchup juu ya burger na
upange tena vitunguu, nyanya, tango na lettice. Baada ya hapo weka
mkate wa burger kwa juu na burger itakuwa tayari kwa kuliwa.
Comments
Post a Comment