Kanye West ajitoa katika mitandao ya kijamii

West alikuwa ameanza kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu na alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono rais Donald Trump.

Image result for kanye west and kim kardashian
Kanye na Kim
Hatua yake pia ilijiri baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba. Hata hivyo mashabiki wengi wanahisi huenda misukumo ya kisiasa na chuki kati yake na mwanamuziki mwenzake J ay zee yaweza kuwa sababu ya yeye kujitoa kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram ambazo zilikuwa na mamilioni ya wafuasi.
Sababu hazijulikani lakini mwezi Novemba mwaka jana alimaliza ziara yake mapema dunia kuliko jinsi watu walivyozoea.
Alimshtumu mwanamuziki mwenzake Jay Z kwa kujaribu kumuua na kuondoka katika jukwaa baada ya kutangaza kwamba atampigia kura rais wa Marekani Donald Trump wakati wa uchaguzi wa taifa hilo.
Mkewe nyota wa Reality TV Kim Kardashian bado yupo katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51.
 Amekuwa akijikuza pamoja na kampuni ya kuuza nguo ya mumewe.
Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake.
Mashabiki walimsihi Kardashian amwambie mumewe arudi katika mtandao ila hakujibu chochote.

Comments

Popular Posts