Kwa wanaume utafanyaje ili uonekane nadhifu?

Ikiwa wewe ni mwanaume unayekwenda na wakati na unataka kuonekana nadhifu sana mbele ya macho ya kila mtu, Zingatia yafuatayo;
1.MAPELE USONI, ni tatizo kwa wanaume wengi na wanafikiri ni maradhi kumbe ni uchafu
kidevu kinabeba nongo jasho na mafuta yote yanayotiririka usoni hivyo unyoapo zingatia haya
  • usitumie wembe zaidi ya mara mbili
  • safisha kidevu chako kwa maji ya moto kabla na baada ya kushave
  • kiwembe cha kidevuni usikitumie kunyoa kwingineko
  • tumia gillete au bic au brand nyingine yoyote nzuri safisha kidevu kila ulalapo
  • kama una dalili ya mapele kidevuni, kisugue kidevu kwa mswaki laini kisha paka ndimu
  • paka mafuta ya nazi.
2. FUNGUS SEHEMU ZA SIRI,hii husababishwa na uchafu, unaoga mwili wote lakini huko chini unakusahau, fanya hivi kutibu tatizo
Image result for usher in a suit
Usher akiwa nadhifu
  • usivae bukta mbichi au yenye unyevu
  • Nyoa angalau mara mbili kwa wiki.
  • usivae bukta zaidi ya mara moja
  • oga kila ulalapo.
  • kina uogapo sugua kende na maeneo yanayozizunguka kwa kitaulo kisha suuza vema
  • kausha vizuri kisha pak mafuta hasa ya nazi
  • lala uchi au vaa bukta nyepesi kuvipa vifaa nafasi ya kupumua
  • usilale bila kujiswafi ufanyapo ngono.
3. FUNGUS MIGUUNI NA MIGUU KUNUKA, hali ya Tanzania ni ya kitropiki hivyo kuna joto mno, viatu tuvaavyo vingi ni semi leather hivyo kuifanya miguu ipumue mno
fanya hivi
  • jitahiti kuwa na pair zaidi ya moja za viatu
  • usirudie soksi
  • usivae soksi mbichi au nyevu
  • kila uogapo jitahidi kusugua kati kati yavidole kwa kitaulo kidogo
  • hakikisha unakausha miguu vizuri kabla ya kuvaa soksi
  • Related image
    Trey akionekana nadhifu
  • paka mafuta ya nazi. 
4. UVAAJI
  • Vaa nguo zinazokukaa vizuri zisibane sana au kupwaya sana.
  • Vaa nguo safi wakati wote.
  • vaa nguo inayoendana na sehemu au mahali au tukio husika.
  • Vaa viatu vinavyoendana na nguo ulizovaa.
  • Mara zote vaa ukijitazama kwenye kioo ili kuepuka kasoro ndogo ndogo kwenye uvaaji.
 Ukifuata maelekezo haya rahisi utaonekana mwanaume wa kisasa na utapendwa na wanawaka mpaka utashangaa hata kama huna hela.

Comments

Popular Posts