Mark Zuckerberg ala Ugali huko kenya

Mark Zuckerberg akila Ugali na samaki nchini Kenya
Zuckerberg akila ugali samaki

Mwanzilishi wa kampuni ya facebook Mark Zuckerberg mwishoni mwa mwaka jana alizuru nchini Kenya katika ziara yake ya mataifa ya bara Afrika.
Zuckerberg aliyewasili siku ya Jumatano kutoka nchini Nigeria alifanya kikao na waziri wa habari nchini Kenya Joseph Mucheru,ambapo walizungumza kuhusu mtandao na mipango ya serikali kuhakikisha kila kijiji kimeunganishwa na mtandao.
Baadaye Zuckerbag aliekea katika hoteli ya Mama Oliech katika chakula cha mchana ambapo kwa mara ya kwanza alikula Ugali na Samaki.
''Swala muhimu ninapozuru taifa lolote jipya ni kujaribu kula chakula chao.Nilipenda sana ugali na samaki mzima wa tilapia'',alisema Zuckerberg.

Comments

Popular Posts