Mwanamke mnene zaidi duniani hatoweza kutembea tena
Mwanamke mhindi aitwaye Eman Abd El Aty anayedaiwa kuwa na kilo 500 aliondoka hospitali ya
India siku ya Alhamisi baada ya madaktari kusema kuwa amepoteza takriban
kilo 250.
Alisafirishwa kupitia ndege ya abiria hadi Uarabuni.
Madaktari wanasema kwamba atafanyiwa matibabu ya viungo.
Katika wiki chache zilizopita hivi karibuni kulizuka ugomvi kati ya madaktari wake India na familia yake.
Ugonvi huo ulianza baada ya dadake Shaimaa Selim kutoa kanda ya video katika mtandao wa kijamii kwamba dadaake alikuwa bado hawezi kuzungumza ama hata kutembea na kwamba hakupoteza kilo nyungi kama ilivyoarifiwa na hospitali hiyo.
Hospitali hiyo ilikana madai hayo.
Bi Selim alitaka dada yake abaki katika hospitali hiyo hadi atakapoanza kutembea, lakini madaktari wa mifupa katika hospitali hiyo walisema kuwa hatotembea tena kutokana na mifupa yake kushindwa kuhimili uzito wake.
Madaktari na wauguzi walimsindikiza mwanamke huyo hadi Abu Dhabi.
Alikuwa amewasili nchini India kwa kutumia ndege ya kubeba mizigo mnamo mwezi Februari na akawa akinyweshwa maji pekee ili kupunguza uzito wake ili madaktari waweze kumfanyia upasuaji wa kupunguza tumbo lake.

![]() |
Huyu ndie mwanamke mnene zaidi duniani ambaye huenda hataweza kutembea tena. |
Comments
Post a Comment