Ndege zisizo na marubani Zitaanza kubeba abiria mwaka 2020
"Hili linafungua njia ya kustawisha Cormorant kutoka kwa hatua ya
majiribio hadi uzalishaji kamili karibuni na hatimaye kuanza kutumiwa
kibiashara kwa teknolojia hii - kwa shughuli mbalimbali," alisema afisa
mkuu mtendaji wa Urban Aeronautics Rafi Yoeli.
Kampuni moja ya Israel imesema ndege
isiyokuwa na rubani, ambayo ilikamilisha safari yake ya kwanza kabisa
ikipaa juu ya maeneo tambarare mwezi Novemba, huenda ikaanza kutumika
rasmi kufikia 2020.
Ndege hiyo imeundwa na kufanyiwa kazi kwa
kipindi cha miaka 15, lengo likiwa kutumika katika juhudi za uokoaji au
shughuli za kijeshi duniani.![]() |
Hii ndio ndege isiyo na rubani |
Kampuni ya Urban Aeronautics imesema ndege hiyo ina rafadha (mapanga yanayozunguka kwa kasi ili kuendesha chombo) zilizo ndani na hilo linaifanya kuwa salama zaidi kushinda helikopta.
Kandi na kuweza kupaa juu na kutua bila kuhitajika kusonga mbele au nyuma, inaweza kupaa kupitia kati ya majumba na hata kupitia chini ya nyaya za umeme.
Ndege zisizo za rubani zimeanza kupata umaarufu katika kutumiwa kibiashara.
Amazon majuzi walitangaza kuanzishwa kwa huduma ya Prime Air, ambapo ndege zisizo na rubani zinatumiwa kusafirisha bidhaa kwa wateja.
Mwezi Juni, ndege nyingine isiyo na rubani ambayo iliungwa na kampuni ya Ehang kutoka China ilipewa idhini ya kufanyiwa majaribio jimbo la Nevada, Marekani.
Mtaalamu wa ndege zisizo na marubani Ravi Vaidyanathan anasema mafanikio ya safari ya majaribio ya ndege hiyo ya Israel ni ufanisi mkubwa na kwamba ni uamuzi wa busara kwanza kuitumia kwa juhudi za uokoaji na shughuli za kijeshi.
Lakini ingawa huenda muda mfupi baadaye zikatumiwa kwa safari za kiraia - na kusaidia kufika hasa maeneo yasiyo na miundo mbinu au yenye misongamano ya magari - bado ni mapema kujua hilo litatekelezwa kikamilifu linu.
"Kuna changamoto nyingi za kihesheria, mfano kuhusu ni wapi unaruhusiwa kupaa? Ni wapi unaweza kutua? Unaruhusiwa kupaa juu hadi wapi?" alisema.
Wadau watu wataziamini kwel bila maruban
ReplyDelete