Sidiria inayoweza kugundua saratani ya matiti yavumbuliwa mexico
Kijana mmoja nchini Mexico amevumbua sidiria inayoweza kugundua saratani ya matiti.
Lakini je sidiria hiyo inafanya kazi? Na iwapo inafanya ,inafanya vipi?.Juliana Rios Cantu mwenye umri wa miaka 18 ametengeza sidiria ambayo anasema itatoa onyo la mapema kwa mtu mwenye dalili za saratani hiyo.
Sidiria hiyo kwa jina Eva iliotengezwa naye na marafiki zake watatu walianzisha kampuni hiyo pamoja.
Lakini iliwagarimu fedha nyingi ili kuifanyia majaribio na hivi karibuni wakashinda tuzo katika hafla ya wanafunzi wanaotaka kufanya biashara duniani.
Kampuni yao iitwayo Higia Technologies iliibuka mshindi baada ya kuzishinda kampuni nyengine za biashara kutoka kote duniani ili kushinda dola 20,000 kuzalisha wazo lao.
Uvimbe ulio na saratani unaweza kupandisha vipimo vya joto mwilini.
Uwezo wa sidiria ya Eva ni kwamba ina sensa ambazo inaweza kupima viwango vya joto, kuviweka katika programu na kumuelezea kuhusu mabadiliko yanayomsumbua.
Wanawake wanaohitaji sidiria hiyo watalazimika kuivaa kwa dakika 60 hadi 90 kwa wiki ili kupata vipimo vya sawa.
Hii ni awamu ya kwanza ya dalili za ugonjwa huo.
Tayari sidiria hiyo imefanyiwa majaribio na itafanyiwa vipimo vyengine vya kimatibabu kabla ya wataalam wa ugonjwa wa saratani kuipendekeza kuwa njia ya kugundua saratani.
![]() |
Kushoto ni kijana huyo mgunduzi na kulia ni sidiria aliyoigundua. |
Comments
Post a Comment